Screen Reader Mode Icon

Tunamwamini Roho Mtakatifu: Karibu kwenye Utafiti wa Kimataifa wa Kuwa Mlutheri

Mchakato wa Kutafiti juu ya Utambulisho wa Kilutheri: Tunamwamini Roho Mtakatifu: Kutoka 2019-2022, FMKD linajishughulisha na utafiki wa kimataifa wa tambulisho za sasa za Kilutheri katika muktadha wa makanisa ya sehemu husika. Mchakato unafanya tafakari ya nguvu ya kitheologia na fursa za ubunifu kuwa jambo muhumu kwa ajili ya ushiriki wa makanisa hayo. Lengo ni kusikiliza ili kupata undani wa njia ambazo tunazitumia kuelezea utambulisho wa Kilutheri tunaoshiriki pamoja kwa njia ya upatanisho wa tambulisho zetu tunazoishi nazo katika mazingira yetu yanayovuka ushirika wetu. Utafiti huu unachunguza jinsi ubatizo, imani na desturi zinazohusiana na jinsi Walutheri wanavyoona wameitwa kuiishi jadi yetu katika tamaduni na miktadha tofauti.

Njia mbili za kushiriki

Baada ya mashauriano ya mwanzo pale Addis Ababa, tunafungua mazungumzo haya kwa ushirika mzima. Tunatumaini tutapata ushiriki katika ngazi zote za kanisa. Kwa njia mbili za kushiriki, ambazo zimebuniwa kwa ajili ya matumizi tofauti:

1.    Hojaji imebuniwa kwa ajili ya mshiriki yeyote katika kanisa lako ili akupe mrejesho. Askofu, Mchungaji, Mkristo wa kawaida na kijana, mtu yeyote anaweza kuingia kwenye sehemu ya tovuti hii https://fr.surveymonkey.com/r/MCXJG5H ili kushiriki. (Unaweza kusambaza hojaji kwa njia ya mfumo wa mfumo wa "neno" [word format] hapo chini, unaijaza na kuirudisha kwa njia ya barua pepe BeingLutheran@lutheranworld.org.) Hojaji inauliza maswali kuhusu imani, desturi, na namna utambulisho wa Kilutheri unavyohusiana na maisha yako ya kila siku..

2.    Mwongozo wa mjadala ulioambatanishwa ni nyenzo ya kukusaida kusaidia wewe mhusika kufungua mazungumzo yenye mwongozo katika ngazi mbalimbali katika kanisa lako. Sharika zinaweza kutumia mwongozo kuandaa mazungumzo miongoni mwa wajumbe wa halmashauri zake, madarasa ya watu wazima, kikundi cha vijana, au washarika binafsi ambao wanataka kutafakari kwa undani zaidi. Katika ngazi ya kidayosisi au kitaifa, vikundi vya wachungaji au watumishi vinaweza kujadili pamoja kuhusu maswali haya. Katika taasisi ya kitheologia, mazungumzo yanaweza kuandaliwa miongoni mwa wanafunzi. Tafadhali tuma hivi vyanzo, kwa lengo la kuhamasisha mazungumzo katika ngazi ya dayosisi, jimbo, usharika au kigango.

Majibu yako ni muhimu! Habari zinazokusanywa ni njia mojawapo ya sisi kupata uzoefu wa umoja wetu na tofauti yetu katika ushirika. Utatifi ni wa siri, kwa maana kwamba mtu au kanisa linalojibu halitaonyeshwa wakati wa kuchapisha matokeo. Tutahitaji kutunza kumbukumbu ya watu ili kutambua hali ya ushiriki wa jumla wa kikanda na jumuiya, na kuhakikisha kuwa kunakuwa na uwasilishaji wa hojaji moja kwa mtu mmoja. Uchambuzi utachapishwa na kushirikishwa kwa makanisa washirika na walioshiriki katika hojaji.

Utafiti utafanyika kwa miezi mitatu, na mwisho wa kupokea hojaji zilizojazwa ni tarehe 31 Machi 2021. (Majibu ya mwongozo wa utafiti yatapokelewa hadi tarehe 30 Juni 2021) Asante kwa kuchukua muda wako kushiriki katika mchakato huu wa kusikiliza. Maswali, na pia majibu yatumwe kwa mfumo wa Neno (Word format) kwa njia ya barua pepe kwa BeingLutheran@lutheranworld.org
0 of 21 answered
 

T