Utafiti wa Mahitaji ya Makazi ya jamii

Karibu!

Asante kwa kushiriki katika utafiti huu wa umma - maoni yako ni muhimu sana. Utafiti huu unafanywa na Tume ya Wilaya ya Mipango ya Thomas Jefferson na Jiji la Charlottesville ili kuelewa vizuri mahitaji ya jamii kama yanavyohusiana na upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, Kutobaguliwa unapotafuta Makazi, na maboresho na huduma za umma ndani ya Jiji la Charlottesville, Albemarle, Louisa, Fluvanna, Greene, na kaunti za Nelson.

Majibu yako ni ya hiari na hakuna atakayejua kwamba ni wewe ndiye uliyejibu. Hakuna atakayejua kwamba haya ni majibu ya mtu binafsi, na data zote zitaandaliwa na kuchambuliwa kwa jumla.

Tunajua kwamba muda wako ni wa thamani. Utafiti huu unapaswa kuchukua takriban dakika 10 kukamilisha. Ushiriki wako unathaminiwa sana.
1.Ninaishi
2.Tafadhali chagua chaguo bora linalokuwakilisha.
3.Je, una umri wa miaka ngapi?
4.Je, wewe ni wa asili ya Wahispania, Walatino, au Kihispania?
5.Je, unaweza kijitambulisha kama nani? Tafadhali tia alama kwenye majibu yote yanayohusika.
6.Ikiwa ni pamoja na wewe mwenyewe, je, watu wangapi wanaoshi nyumbani kwako?
7.Je, makadirio ya wastani wa mapato ya kila mwaka ya wanafamilia wako (jumuisha wanafamilia wako wote)?
8.Je, jibu gani linaelezea bora kuhusu hali yako ya maisha ya sasa kati ya majibu yafuatayo?
9.Tafadhali kadiria kiwango cha umuhimu wa masuala yafuatayo kwako na jamii yako.
Si Muhimu Hata kidogo
Si Muhimu
Sipendelei upande wowote
Muhimu
Muhimu Sana
Nyumba za Bei nafuu
Uboreshaji wa Miundombinu ya Umma: Kukarabati mitaani, Vifaa vya usalama
Maendeleo ya Kiuchumi, Maendeleo ya Kibiashara, na Kutoa Fursa za Kazi
Huduma za Kijamii na Huduma za Msaada
10.Tafadhali chagua huduma tano (5) ambazo zitakufaidika wewe na jamii yako zaidi.
11.Kwa maoni yako, je, wewe na jamii yako mnahitaji nini zaidi? Tafadhali chagua tano (5).
12.Tafadhali chagua mahitaji matatu (3) makubwa ya kiuchumi katika jamii yako.
13.Tafadhali onyesha kwamba mambo haya yanahitajika kwa kiwango gani, ukizingatia hasa mahitaji ya mtu asiye na makazi.
Hayahitajiki Sana
Yanahitajika kwa Wastani
Yanahitajika Sana
Yanahitajika Kabisa
Mafunzo ya kazi
Usimamizi wa kesi/ujuzi wa maisha
Matibabu ya madawa ya kulevya
Huduma ya afya ya akili
Huduma ya afya ya kimwili
Kupewa makazi
Fursa za elimu
Utatuzi wa migogoro/mizozo
Msaada wa kisheria
14.Je, wewe au mtu unayemjua amekabiliwa na changamoto zozote zifuatazo zinazohusiana na makazi? Tafadhali tia alama kwenye majibu yote yanayohusika.
Mifano ya Ubaguzi:
  • Kukataa kumuuzia mtu au kupangisha nyumba kwa sababu ya utambulisho wake (kwa msingi wa mbari, rangi, asili ya taifa, dini, jinsia, hali ya familia, na/au ulemavu).
  • Kuchapisha taarifa inayoashiria kwamba unapendelea au haupendelei watu wanaojitambulisha kwa njia fulani.
  • Kumwambia mtu kuwa nyumba haipatikani, hasa kwa sababu ya utambulisho wake.
  • Sehemu zilizoandikwa za hati ya makubaliano au ya kukodisha zinazowazuia watu wa utambulisho fulani kupata nyumba hiyo.
  • Kutoa masharti tofauti au upendeleo kwa wapangaji au wanunuzi tofauti kulingana na utambulisho wao.
15.Sheria ya Makazi ya Haki ya Serikali ya Shirikisho inakataza ubaguzi katika uuzaji, kukodisha, na kupeana mikopo au rehani ya nyumba kwa msingi wa mbari, rangi, asili ya taifa, dini, jinsia, hali ya familia, na ulemavu. Je, unafikiri kwamba aina gani ya ubaguzi wa makazi ni ya kawaida sana katika eneo letu kati ya hizi?
16.Je, unaweza kumwelekeza mtu akwende wapi akibaguliwa anapojaribu kupata nyumba?
17.Je, wewe au mtu unayemjua amewahi kubaguliwa katika suala la makazi katika maeneo haya yoyote yafuatayo?
Nimewahi kubaguliwa
Najua mtu ambaye amewahi kubaguliwa
Kukodisha fleti
Kutafuta nyumba ya kununua
Kupata rehani
Kurekebishiwa mazingira au hali ipasavyo kwa ajili ya ulemavu
Kupata bima
18.Je, wewe au mtu unayemjua aliripoti kuhusu ubaguzi huo?
19.Je, unahisi kwamba unajua kuhusu sheria za ubaguzi wa makazi kwa kiasi gani?
20.Je, unajua kuhusu Sheria ya Kutobaguliwa unapotafuta makazi na Sheria ya Makazi ya Haki ya Virginia (ambayo ni sheria inayokataza ubaguzi kwa msingi wa utambulisho / vikundi vya watu wanaolindwa walioelezwa hapo juu wakati wa kuuza au kukodisha nyumba)?
21.Ikiwa jibu ni “Ndiyo”, ulijifunza wapi kuhusu sheria hizi?
“Makazi ya haki” yanamaanisha kuzuia ubaguzi katika kuuza au kukodisha nyumba.
22.Je, umewahi kufunzwa kuhusu makazi ya haki?
23.Ikiwa jibu ni “Ndiyo”, ni nani aliyekufunza?
24.Kutoka kwenye orodha iliyo hapa chini, kuna maeneo yoyote katika kanda yetu ambayo unaamini kuwa ina matatizo ya ubaguzi wa makazi? Tafadhali tia alama kwenye majibu yote yanayohusika.
25.Je, unajua kuhusu mazoea au vikwazo vyovyote vyenye mashaka ya makazi ya haki katika maeneo haya yoyote yafuatayo?
Ninajua
Siju
Sera za matumizi ya ardhi
Sheria za kugawa maeneo
Viwango vya kumiliki ardhi au kanuni za afya na usalama
Mortgage mikopo au mwezi wa kwanza wa kodi/amana za usalama
Ufafanuzi:

Sera za matumizi ya ardhi — sheria zinazoonyesha jinsi kipande cha ardhi kinaweza kutumiwa na mmiliki wake

Sheria za kugawa maeneo — sheria kuhusu aina gani ya majengo yanaweza kujengwa kwenye kipande fulani cha ardhi. Kama sheria hizi ni haki, hiyo inaweza kuwa ubaguzi. Mazoea ya shaka au ya kibaguzi yanaweza kutenganisha aina maalum za maendeleo kulingana na hoja za kiholela au za kibaguzi.

Viwango vya umiliki/kanuni za afya na usalama - sheria zinazowazuia familia fulani kupata makazi salama. Kwa mfano, sheria ambazo haziruhusu familia zilizo na watoto kuishi katika jengo fulani ni kinyume cha sheria. Kanuni za afya na usalama zinazowabagua watu walio na hali fulani za afya pia zinachukuliwa kuwa kizuizi cha makazi ya haki. Kama mtu hatakukubalia ukodishe nyumba yake kwa sababu ya afya yako au matatizo ya afya ya akili, jambo hilo linaweza kuwa kinyume cha sheria.

Rehani/amana za mikopo - Mazoea ya kukopesha yanayobagua watu binafsi kwa misingi ya mbari, jinsia, asili ya kitaifa, uzee, hali ya familia, ulemavu, chanzo cha fedha, mwelekeo wa kijinsia, au hali ya kijeshi ni kinyume cha sheria. Ikiwa mkopeshaji au benki inakutoza pesa zaidi kwa sababu ya mbari, kundi, umri, ulemavu, ulipozaliwa, au aina ya familia yako, jambo hilo ni kinyume cha sheria.
26.Tafadhali chagua masuala matano (5) ya makazi yanayohitaji kushughulikiwa zaidi katika jamii yako.
27.Tafadhali chagua mahitaji matatu (3) muhimu zaidi kwa ajili ya makazi ya KUKODISHA katika jamii yako.
28.Chagua mahitaji matatu (3) muhimu zaidi kwa ajili ya makazi ya WENYE NYUMBA katika jamii yako.
29.Tafadhali bainisha kuwa watu hawa maalum waliotajwa hapa chini wanahitaji makao kwa kiwango gani.  Unaweza kutumia jedwali la mapato lililo hapo juu kujibu swali hili
Hawahitaji Sana
Wanahitaji kwa Wastani
Wanahitaji Sana
Wanahitaji Kabisa
Wazee
Watu wasio na makazi kwa muda mrefu
Watu wanaotawaliwa na madawa ya kulevya/pombe
Watu wenye ugonjwa wa akili
Waathirika wa vita nyumbani
Watoto walionyanyaswa
Watu wenye VVU/UKIMWI
Familia kubwa (watu 5 au zaidi)
Mapato ya chini sana (angalia hapo juu)
Mapato ya chini hadi ya wastani (angalia hapo juu)
30.Tafadhali toa maoni yoyote ya ziada.