Health Equity Zone Initiative (Mpango wa Eneo la Usawa wa Afya) unasaidia jumuiya katika kutambua masuala makuu ya afya na kukuza miradi ya kutatua mahitaji yao maalum. Katika miaka miwili ijayo, jumuiya yetu ya South King itapokea ufadhili wa kuendesha miradi iliyotambuliwa na jumuiya. Tungependa kusikia matumaini yako kwa jumuiya yetu! Shiriki mawazo yako na ujiunge nasi katika kuunda jumuiya salama zaidi kwa wote.